Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa TLS na Mwanasheria wa CHADEMA amekua akishikiliwa na Polisi kwa siku mbili ambapo ilidaiwa na CHADEMA kwamba ni makosa mawili yaliyofanya akamatwe likiwemo moja la uchochezi.
Taarifa za jioni hii ni kwamba Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana na Polisi baada ya kumshikilia kwa hizo siku mbili tangu alipokamatwa ghafla August 22, 2017.
Licha ya kupewa dhamana pia Lissu amepewa masharti ambapo Wakili wake Peter Kibatala amesema amepewa masharti ya kurudi katika Kituo Kikuu cha Kati August 28, 2017.
Lissu alikamatwa August 22, 2017 wakati anatoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza shughuli za Mahakama ikiwa ni pamoja na kusimamia kesi ya makosa ya kimtandao inayomkabili Yericko Nyerere.