unnamed (1)
UONGOZI wa Azam fc umewarejesha kambini wachezaji wake wawili kabla ya kumaliza adhabu waliyopewa ya kufungiwa mechi nne kwa kosa la kuondoka kambini bila kuaga.Kipre Tchetche na Aggrey Morris walifungiwa mechi nne kuanzia ile ya sare ya 1-1 na Mbeya City, 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na 0-0 na Mgambo JKT, lakini wamerejeshwa kuelekea mechi ya nne katika kifungo chao dhidi ya Kagera Sugar hapo kesho uwanja wa Azam Complex.
Azam wanashika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 39 katika mechi 21 walizocheza, pointi saba nyuma ya vinara Yanga waliocheza mechi 21 pia.

Katika sare tatu walizopata mfululizo, safu ya ulinzi ilicheza hovyo baada ya kumkosa Aggrey Morris ambaye anacheza vizuri na Paschal Wawa, lakini safu ya ushambuliaji pia iliyumba kwasababu Didier Kavumbagu alikosa mtu sahihi ambaye ni Kipre Tchetche.
Mechi dhidi ya Mgambo, Kavumbagu alicheza na Gaudence Mwaikimba ambaye dhahiri ameshaisha kiuchezaji kwasabbau ya umri na kutopangwa kabisa msimu huu.
Naye Wawa alicheza na Mwantika dhidi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar, lakini waliyumba kwasababu hayuko imara.
Uongozi wa Azam ulitangaza kuwa Kipre na Morris ni majeruhi wakati sio na mtandao huu ukawashauri kuwaponya kiaina na kuwarudisha kambini na imekuwa hivyo.
Muda huu vijana hao wapo kambini Chamazi wakiwasubiri Kagera Sugar kesho ambayo hawakustahili kucheza kama uongozi ungeendelea kushikilia msimamo wake.