CHADEMA WASHINDA KATA YA KIRUMBA MJINI MWANZA NA KATA YA LIZABONI MJINI SONGEA


Uwanja wa furahisha Mwanza wananchi wa kirumba kwa maelfu wakisubiri kutangaziwa ushindi wa diwani baada ya kuishinda CCMM polisi na magari yao kwa wingi muda mfupi uliopita. 

Taarifa zilizotufikia hivi sasa kutoka katika chanzo chetu kinasema kuwa katika Uchaguzi wa Udiwani kata ya Kirumba Mwanza Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kinaongoza kwa  kupata kura 2938 za kura zote zilizopigwa huku wapinzani wao Wa Jadi CCM wakipata Kura 2131. Kwa Kura hizo Basi CHADEMA inaweza kushinda nafasi hiyo ya Udiwani

Na kutoka Mjini Songea vilevile CHADEMA iweza kushinda nafasi hiyo ya Udiwani japokua hatukupata idadi ya Kura ambazo kila chama imepata.'
Lukaza Blog