Sunday, March 25, 2012

Simba wanaongoza goli 2 Es Satif hawajapata kitu mpaka sasa mpira unaendelea

Mshambuliaji wa Timu ya Simba,Salum Machaku (kulia) akijiandaa kuachia shuti kali kuelekea langoni mwa timu ya Es Satif katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Timu ya Simba SC inaongoza goli  2 wakati Es Satif hawajapata kitu mpaka sasa,Goli la kwanza limefungwa na mchezaji Emmanuel Okwi na goli la pili limefungwa na Haruna Moshi a.k.a Boban.
 Mshambuliaji wa Simba,Emmanuel Okwi (kulia) akimtoka beki wa timu ya Es Satif ya nchini Argeria,Farouk Belkaid katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Es Satif
 Marefarii na Manahodha wa timu zote mbili.
 Mkono wa kheri kabla ya mtanange kuanza.
 Ameir Maftah wa timu ya Simba (kulia) akiachia shuti kali kuelekea langoni mwa timu ya Es Satif.
 Beki wa Es Satif (alielala chini) akiondosha hatari langoni mwake wakati Salum Machaku akitaka kujaribu kufunga goli.
 Holaaaaaa..........
 Hatari langoni mwa Es Satif.
Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Fredrick Sumaye (mwenye suti),Waziri wa Afrika Mashariki,Mh. Samuel Sitta (kulia),Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe pamoja na Mbunge wa Tabora Mjini,Mh. Aden Rage wapo uwanjani hapa kuisapoti timu ya Simba.
 Mashabiki wa Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapa.

leo hapatoshi uwanja wa taifa kati ya simba sc na Es Setif ya Algeria

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
Pichani ni kundi la Wanachama wa Simba  kutoka Makao Makuu wanajiita "SIMBA SPORTS CLUB MAKAO MAKUU TAWI LA MAENDELEO" Hapa ni shamra shamra zinazoendelea nje ya uwanja wa taifa kabla ya kuingia uwanjani hivi punde.

Leo ndio leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam pale Simba inapokutana na ES Setif kutoka Algeria katika mchezo wa Kombe la Shirikisho. Simba inarekodi nzuri ya kuwafunga warabu hao kutoka Algeria. Hadi sasa inarekodi ya 3-0.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time promotions Ltd ambao ndiyo waratibu wa mchezo huo ,Bw.Godfrey Kusaga akizungumza na Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage kuhakikisha kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa na Mashabiki wanaingia uwanjani bila matatizo.

 Wewe....nini picha zote hizo..!!!Hapa akimkoromea mpigapicha kwanini anampiga picha nyingi....hahaha alipogundua ni Father Kidevu akabaki anacheka.
Mashabiki wakiwa tayari uwanjani kwa utulivu mkubwa wakisubiri game kuanza na mnyama kumrarua mwarabu. Father Kidevu Blog ipo Live kukurushia mtanange huu wa Simba na ES Setif kutoka Algeria.

jicho la camera ya jiachie nje ya jiji la dar

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
 Mteja akiulizia bei ya nyanya,ndoo moja inauzwa shilingi 8000/= 
 Urithi wetu wa kujivunia ndani ya hifadhi ya Wanyama Mikumi.
 Mdau nae akikimbiza mpango mzima mapema sokoni ndani ya Iringa.
 Nchi yetu nzuri ya milima na mabonde ya kuvutia
 Unajua ni kwanini nazi inavunjiwa sokoni na si mara baada ya kufika nyumbani kwa matumizi.
Mchicha bila maji hauuziki;Mama akiwa na mtoto wake akiuza mboga mboga soko kuu la mjini Iringa hivi karibuni.

semina elekezi ya msimy wa mashindano ya ya copa coca cola 2012 yafunguliwa jijini dar

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
Mkurugenzi wa Michezo katika wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina elekezi ya msimu wa mashindano ya Copa Coca Cola 2012 kwa Makatibu wa vyama vya Mikoa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni wa Rais wa Shirikisho la Soka (TFF) Athuman Nyamlani na Meneja uhusiano na Makamu Mawasiliano wa Kampuni ya Coca-Cola Kwanza,Evance Mlelwa.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka (TFF) Athuman Nyamlani,akizungumza wakati ufunguzi wa semina elekezi ya msimu wa mashindano ya Copa Coca Cola 2012 kwa Makatibu wa vyama vya Mikoa jijini Dar es Salaam jana mashindano ya Copa Coca Cola 2012 kwa Makatibu wa vyama vya Mikoa jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni  Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari  Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo na Meneja uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Coca-Cola kwanza,Evance Mlelwa.

Mkurugenzi wa Ufundi na Afisa Maendeleo wa Shirikisho la Soka(TFF) Sunday Kayuni,akizungumza wakati ufunguzi wa semina elekezi ya msimu wa mashindano ya Copa Coca Cola 2012 kwa Makatibu wa vyama vya Mikoa jijini Dar es Salaam jana .

rais kikwete amteua Kibelloh kuwa Mwenyekiti KADCO

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
Na mwandishi wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemteua Balozi mstaafu wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni inayosimamia maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO).

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi leo inasema kuwa uteuzi huo ulianza kazi toka mwezi Machi tarehe 15. Aidha, taarifa hiyo pia ilisema kuwa Waziri wa Uchukuzi, Mh. Omari Rashid Nundu kwa mamlaka aliyonayo amewateua wajumbe wanne wa bodi ya wakurugenzi ya KADCO. Wajumbe hao wanne ni pamoja na Seleman O. Seleman, Andrew Nyumayo, Mwajuma Mwanilwa na van de Kreeke ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO.

Uteuzi huo wa bodi umekuja wakati KADCO ikiwa katika mipango ya uboreshaji na ukarabati wa Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuwa uwanja wa ndege unaowezesha ndege kubwa za kimataifa kutua.

Kampuni ya KADCO imepata mkopo wa dola za kimarekani 35 milioni (zaidi ya 47 bilioni) kutoka kampuni ya nchini Uholanzi, Orion Grand Facility. Mkopo ambao utasaidia katika ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege na maeneo mengine muhimu ya uwanja.

Hivi karibuni, Qatar Airways ilitangataza mpango wa kutua katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa kutumia ndege kubwa ya A320 kupitia Nairobi, Kenya kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

Mashirika mengine ya ndege yanayotumia uwanja wa KIA ni pamoja na KLM, Edelweiss Air, Condor Air na Shirika la Ndege la Ethiopia. 

Katizo la umeme DSM, maeneo yatakayokatizwa Jimbo la Ubungo

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
Jumapili tarehe 25 Machi kutakuwa na katizo la umeme kwenye baadhi ya maeneo ya DSM kuanzia saa 2 Asubuhi mpaka  10 jioni.
Kwa Jimbo la Ubungo katizo litahusu maeneo yafuatayo: Sinza, Goba, Ubungo Kisiwani, Mabibo Jeshini,  Makuburi (External, Barabara ya Mandela, Mabibo Hosteli, Kibangu).
Hivyo usishike waya wowote uliokatika badala yake toa taarifa kwa ofisi za kanda za TANESCO Kinondoni Kaskazini (Mikocheni):0716768584; 0784768584 au Kinondoni Kaskazini (Magomeni): 0768985100; 0784271461; 0784078837 au 0788379696.
Sababu zilizotajwa na TANESCO: Kuunga line ya msongo mkubwa wa 132kV katika kituo cha kupoozea umeme Ubungo na Kufunga LBS kwenye njia ya FZ3-1&2 na U1 ili kurahisisha uzimaji wa line wakati inapopata hitilafu na kurahisisha kugundua eneo la hitilafu kwa urahisi na haraka. Maslahi ya Umma Kwanza.

Mh Zitto Kabwe:Kwanza niseme wazi kabisa kabisa kuwa Urais ninautaka.

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
Ninaamini ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini nina uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili wa namna nchi yetu inavyoongozwa. Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content). Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika.
Ninajua nchi yetu inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). Ninajua ‘transformation’ inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu. Ninajua rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi, Ardhi n.k. ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu.
Hivyo, nchi inahitaji Kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi. Sio kazi rahisi lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye. Mimi nataka kuifanya. Nina uwezo wa kuifanya.
Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii. Ni lazima Watanzania wengi waseme wewe ndio mwananchi mwenzetu unayeweza kuchukua jukumu hili. Kuitaka tu haitoshi. Ni lazima wananchi wakuamini na kukupa jukumu hili.
Sasa kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au hata 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo.
Mjadala wa umri wa kugombea Urais imekuwa mjadala mkali sasa. Mjadala huu baadhi ya watu kwa sababu wanazojua wao wameamua kuita ni mjadala wa Zitto na January. Kwamba ni mjadala unaobagua Wazee. Mjadala unaopandikiza chuki na sumu za kibaguzi. Kwamba ni mjadala wa Kitabaka na kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi. Sitamsemea January, nitajibu baadhi ya hoja za mwandishi wa makala mojawapo kama Zitto. January akitaka atamjibu naye kivyake.
Mwandishi anasema yeye hapingi hoja ya umri, bali anapinga aina ya watu wanaoshadidia hoja hiyo. Anaipenda hoja ila hapendi watoa hoja. Hoja nzuri lakini Zitto na January wabaya. Amelisema hilo mwanzo kabisa wa makala yake. Kwa hiyo kwake yeye hoja ingeletwa na vijana wengine asingekuwa na shida wala isingekuwa hoja hatari. Kwa kuwa hoja imeletwa na Zitto na January (ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii) ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa sana wasomi wa siku hizi. Wasomi wanaojadili watu badala ya masuala.

Mahojiano na Anna Mwalagho

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
Kazi yetu ni kutunza kumbukumbu za wale ambao wanathamini mawazo fikra, mbinu zao kwa manufaa yawengine au vizazi vipya.

Msikilize kwa makini Muigizaji, Mchezaji, Mshairi, msimulizi wa hadithi na mwimbaji Anna Mwalagho akieleza mengi kuhusu maisha yake. Ameeleza alivyoanza mpaka alipofikia, waliomvutia, mafanikio katika kazi na mengine mengi.

Msikilize kwenye mahojiano haya aliyofanya nasi ndani ya studio za Asparagus zilizopo Takoma Park, jimbo la Maryland nchini Marekani

Balozi wa Ireland atembelea Kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL)

Sunday, March 25, 2012 Maoni: 0
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (katuikati) akimsikiliza Brewery Manager wa SBL Colman Hanna juu ya hatua mbalimbali za uzalishaji bia SBL. Kulia ni Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (kushoto) akitoka baada ya kumaliza ziara hiyo kiwandani hapo. Pamoja nae ni Brewery Manager wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Colman Hanna na Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins anaeonekana kwa nyuma.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (wapili kulia) Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins, Brewery Manager wa SBL Colman Hanna, Meneja  Mawasiliano wa SBL, Imani Lwinga na Meneja wa Ubora wa SBL, Alloyce Nduka wakionja bia za SBL wakati wa ziara hiyo ya Balozi.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (kushoto) akitembezwa katika kiwanda na Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins (kulia) na Brewery Manager wa SBL Colman Hanna.

Saturday, March 24, 2012

MBIO ZA KUMPATA MISS UTALII KINONDONI 2012 ZAANZA

Saturday, March 24, 2012 Maoni: 0
Miss Tourism Tanzania Organization – Kinondoni, wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Kinondoni,wametangaza nafasi kwa mabinti wenye sifa za kushiriki Miss Utalii Kinondoni 2012 kujitokeza kujaza fomu za kuomba kushiriki mashindano hayo,yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa Aprili 2012 wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini, mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Organisation wilaya ya Kinondoni,Ndugu Pius Yalula, amesema kuwa fomu hizo zitaanza kutolewa siku ya Jumatatu Tarehe 26-3-2012 katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na Zizzu Fashion ( Victoria) ,BM Saloon ( Kinondoni), Sea Boys Internet Café ( Magomeni), Aucland Tours & Safaries ( Maeneo ya Posta), Ofisi za Mlonge By Makao ( Pamba House Posta), Katika Ofisi za Miss Tourism Tanzania Organization ( Ilala Bungoni), Dar es Salaam City Collage ( Kimara), Kumekucha Action Mart (Sinza)COCO Beach Oyster bay na TINTONA TANKSTATION ( Kinondoni Manyanya). Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni tarehe 12-4-2012, kabla ya kuanza kwa kambi ya mazoezi kati kati ya mwezi huo April 2012.

Mkurugenzi huyo wa wilaya wa mashindano hayo,alibainisha kuwa sifa za washiriki kwa mujibu wa kanuni na Taratibu za mashindano ya Miss Utalii Tanzania ni pamoja na , washiriki kuwa na Elimu isiyo pungua kidato cha sita au yenye kulingana nayo, umri usio pungua miaka 18-27, Urefu wa angalau sentimita 168 au zaidi, wenye rangi na maumbile asili, Wenye afya njema kimwili na kiakili, wasio olewa wala kuwahi kuzaa, raia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria. Wenye tabia njema,mwenendo mwema , mfano wa kuigwa na tegemeo katika jamii kimaadili na hulka.

Washindi wa shindano hilo watawakilisha na kupepelusha Bendera ya Wilaya ya Kinondoni katika fainali za mkoa  wa Dar Es Salaam , zitalazo wakutanisha washindi hao na washindi wenzao wa wilaya za Ilala na Temeke zitakazo fanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2012, wakichuana kuwania taji la Miss Utalii Dar Es Salaam 2012. Jumla ya warembo 24 watashiriki fainali za Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni nane kutoka kila wilaya.

Kwa niaba ya kamati ya maandalizi wilaya ya Kinondoni 2012, natoa wito kwa mabinti wenye sifa na uzalendo wa dhati kwa wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki, ikiwa ni fulsa ya pekee kwao kuunga mkono juhudi za serikali na Taifa katika kutangaza na kuhamasisha Utalii,Utamaduni,Matumizi ya Bidhaa za na Huduma za Tanzania, Mianya ya Uwekezaji na pia kuhamasisha vita dhidi ya Uharibifu wa Mazingira,Uwindaji Haramu,Uvuvi Haramu,Ujinga,Umasikini,Maradhi, Mila kongwe na Potofu.

Aidha tunaomba watu binafsi, makampuni na mamlaka za serikali za Wilyaya ya Kinondoni kujitokeza kudhamini shindano hili,likiwa ni shendano pekee nchini lisilo husisha mavazi ya kuogelea ,wala mavazi yasiyo ya asili ya Tanzania ambalo litatoa fulsa ya pekee kwa wafanya bishara,makampuni na Wilaya kujitangaza kiuchumi,kitalii,kiuwekezaji na kijamii kitaifa na kimataifa.Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa, hazina na benki kubwa ya Utamaduni wa Tanzania kwa faida ya sasa na baadae.

Wilaya ya Kinondoni , ndiyo inayo shikilia taji la Miss Utalii Dar es Salaa 2011, na taji la Miss Utalii Tanzania 2011 – Mshindi wa Tano, ambapo Mrembo Sofia Dio ndiye anaye shikilia mataji hayo na ndiye atakaye kabidhi taji kwa mrembo mpya wa Miss ?Binti Utalii Kinondoni 2012.

Asante,

Pius Yalula
Mkurugenzi Miss Utalii Kinondoni
Nakala:
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano Miss Tourism Tanzania Organisation

Uandishi wa Kitabu cha Marehemu Regia Mtema (Biography)

Saturday, March 24, 2012 Maoni: 0
Kamati Teule iliyochaguliwa kuanzisha Taasisi ya Regia Mtema Foundation imedhamiria kufuatilia kuandikwa kwa kitabu cha Marehemu Regia Mtema kufuatia azimio lililoafikiwa katika kikao cha kwanza cha Marafiki wa Regia pale British Council na baadaye kuwekewa uzito katika kikao cha Kamati Teule. 

Kamati Teule sasa inapenda kutoa fursa ya kualika mtu au kampuni yeyote ambayo inaweza kuifanya kazi hiyo ya uandishi kwa uharaka, ustadi na ubora wa hali ya juu. Itahitajika kujua mchanganuo wa gharama zote za zoezi zima.

Kazi hii inatarajiwa itahusisha kuweka kumbukumbu ya historia ya Regia, Kazi mbalimbali alizofanya, picha nk. nk.

Kama wewe ni mojawapo wa waandishi wa Biography au unamfahamu yeyote, tafadhali naomba tuwasiliane moja kwa moja kupitia barua pepe sam@danimex.com. 

Application Open for a Film Master Class Workshop

Saturday, March 24, 2012 Maoni: 0
Dear alumni and filmmaking friends!
Please forward this mail to anyone you may know who may benefit from our Masterclass Filmmaking Workshops.
We want the widest range of applications possible. Pls support us support your community. Pay it forward & send this to everyone you know!!!!!!
Dear all
A reminder we are open for applications for our annual Master class Film Training Workshops www.onefinedayfilms.com
This is our fourth year! There are two aspects.
1. The 2 week Master Class Classroom Filmmakers Workshops.

These are June 18th to June 29th 2012.
They have previously been held in Kenya, for the 60 participants invited to attend from all over Africa. This year we may be hosting the workshops in another location (Zanzibar, Kampala, Arusha, Kigali are being considered).
We cover all travel and accommodation costs for successful candidates. There is no charge for the course.
There are EIGHT departments


1.      Cinematography


2.      Directing


3.      Editing


4.      Film composing (NEW!!!!)


5.      Production


6.      Production design / art department


7.      Scriptwriting


8.      Sound

These classes are conducted by world class filmmakers from Europe and the USA (last year we had a delegation from the Oscars who came to teach)
2. The Feature film. This will be shot October / November 2012. It is a 4 week shoot.
Priority for all crew selected is given to those attending the two week classroom workshop. We are not yet confirmed which country we will shoot in, but it will likely be Kenya.
This is  a Master class training so you should have an armful of experience to apply, and you must attend all days.  And you cannot possibly be too experienced!

The application consists of THREE PARTS:
1.      A completed Application Form to be emailed to application@onefinedayfilms.org
2.      A 1 minute application video about yourself uploaded to YouTube (the URL of uploaded content to be stated in the Application Form).
3.      A1 minute application video on your previous work, work sample, show reel, etc uploaded to YouTube (the URL of uploaded content to be stated in the Application Form).
 Application forms are available on. www.onefinedayfilms.com
Closing date 25th March. Only complete applications will be considered.
Email us if you have any questions – but please do not send me your application forms and materials!
Lastly please pass this on to your filmmaker friends all over Africa.
Remember - we will cover all travel costs for participants and want this to be a truly Pan African programme.


Thanks!

wizar ya afya yaimarisha hatua mbalimbali za kudhibiti maambukizi shirikishi ya kifua kikuu na ukimwi

Saturday, March 24, 2012 Maoni: 0
Na. Catherine Sungura-Masasi 
 24/03/2012 TB-Kitaifa.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeimarisha hatua mbalimbali za kudhibiti maambukizi shirikishi ya kifua kikuu na ukimwi ikiwa ni pamoja na kuchunguza kila mgonjwa wa kifua kikuu kama ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) katika kila kituo cha afya na hospitali zote nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda kwenye hotuba yake kwenye Kilele cha maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yaliyofanyika wilayani hapa. Dkt. Mponda alisema katika kutekeleza hilo wizara yake inafanya uchunguzi, kutoa dawa ya kuzuia kifua kikuu kwa watu wanaoishi na VVU pamoja na dawa za mseto za kutibu kifua kikuu hivyo kupunguza muda wa matibabu kutoka miezi nane hadi sita .

Alisema asilimia 88 ya wagonjwa wote wa kifua kikuu wanapona baada ya kupata matibabu sahii kwa kutumia dawa mseto,kiwango hicho ni zaidi ya lengo la Shirika la Afya Duniani ambalo linataka kila mwanachama kuponyesha angalau asilimia 85 ya wagonjwa wa kifua kikuu, “hivyo sehemu kubwa wagonjwa wa kifua kikuu wanao uhakika wa kupona baada ya kuanza matibabu hata kama pia wana maambukizi ya VVU.

Hata hivyo alisema Wizara imeanza kununua na kusambaza aina mpya ya darubini za Light Emitting Diode(LED) zenye uwezo mkubwa zaidi wa kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi, hadi kufikia mwisho wa mwaka jana asilimia 80 ya hospitali zote za wilaya zilipata darubini hizo mpya na ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, hospitali zote zikiwemo za mashirika ya kidini zitapatiwa lengo ni kuzipa hospitali zote nchini uwezo mkubwa wa kuchunguza vimelea vya kifua kikuu.

“ Ninaomba watoa huduma kuhakikisha kwamba kila mgonjwa wa kifua kikuu anachunguzwa maambukizi ya VVU baada ya kupata ushauri nasaha na hivyo hivyo wenye maambukizi ya VVU wachunguzwe pia ugonjwa wa kifua kikuu na wale wote watakaobainika wana maambukizi shirikishi wapewe matibabu sahii ikiwemo dawa za kupunguza makali ya virusi mapema iwezekanavyo kulingana na mwongozo wa Wizara”alisisitiza.

Aidha Dkt. Mponda alisema kwa kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya kifua kikuu “ Nitatokomeza kifua kikuu kipindi chote cha uhai wangu” ina lenga watoto ambao ni taifa la kesho wategemee kuishi kwenye ulimwengu ambao hakuna mtu yeyote anaugua kifua kikuu hivyo swala la kutokomeza ugonjwa huu si la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii peke yake bali ni la kushirikisha sekta zote hapa nchini.

Awali Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Ernest Kasoyaga alisema ugonjwa wa kifua kikuu bado ni tatizo kubwa mkoani hapo ambapo takwimu zinaonyesha idadi kubwa ya wagonjwa waliogunduliwa na kupatiwa matibabu mwaka 2009 kulikuwa na wagonjwa (1,902) , mwaka 2010 (1,898), mwaka 2011 (1,907) , na katika wiki hii ya maadhimisho kwa siku sita waliendesha zoezi la kuhamasisha na kupima makohozi kwa wananchi wa wilaya ya masasi katika vituo saba, ambapo watu wapatao 602 waliojitokeza katika zoezi hilo wakiwemo wanaume 287 na wanawake 315 kati ya watu hao watu 25 waligundulika kuwa na vimelea vya kifua kikuu idadi hiyo ni sawa na asilimia 3.6.

Alisema ongezeko hilo la wagonjwa linatokana na maambukizo ya VVU ambapo toka oktoba mwaka 2010 hadi Septemba 2011 kati ya wagonjwa wa kifua kikuu 1,647 waliopimwa VVU, wagonjwa 440 sawa na asilimia 27 waligundulika na Virusi vya Ukimwi.

Rais Kikwete awaapisha Makatikbu Tawala wa Mikoa ikulu jijini Dar Es Salaam

Saturday, March 24, 2012 Maoni: 0

Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Mbeya Bibi.Mariam Mtunguja akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo Rais aliwaapisha pia makatibu Tawala wa mikoa mingine kama ifuatavyo,Dkt. Faisal Issa(Kilimanjaro),Bwana Eliya Ntandu(Morogoro), Bwana Severine Kahitwa(Geita),Bwana Emmanuel Kalobelo(Katavi), Bwana Hassan Bendeyeko(Ruvuma) na Dkt. Anselem Tarimo (Shinyanga)(Picha na Freddy Maro).

serikali ya china yaipa mkopo nafuu na msaada Tanzania zaidi ya bilioni 80

Saturday, March 24, 2012 Maoni: 0
Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (kulia ) akisaini kitabu cha wageni cha Wizara ya Fedha leo jijini Dar es salaam wakati alipokwendakusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali inayozidi shilingi bilioni 80. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(hayupo pichani)kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao  
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (kulia) wakisaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Serikali ya China kuipa mkopo nafuu na msaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo nchini. Msaada na mikopo hiyo ni zaidi bilioni 80 fedha za Kitanzania ambayo inazidi kuimarisha urafiki na undugu kati ya Tanzania na China. 
Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (aliyesimama ) akitoa hotuba jana jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya kuisaidia Tanzania. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (hayupo pichani)kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao. Kulia ni Balozi wa China nchini Lu Youqing.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(aliyesimama ) akitoa hotuba jana jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri Mkulo kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (hayupo pichani) . Msaada na Mkopo huo unazidi bilioni 80 Fedha za Kitanzania. Kushoto ni Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu na kulia ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (kulia) leo jijini Dar es salaam wakati kiongozi huyo alipokwenda Wizara ya Fedha kwa ajili ya kusaini mkataba wa mkopo nafuu na msaada wa zaidi ya bilioni 80 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.

KAMPUNI YA ALLIANCE ONE TANZANIA YAWAELIMISHA WAHARIRI JUU YA ZAO LA TUMBAKU

Saturday, March 24, 2012 Maoni: 0

Mkurugenzi wa Alliance One Tanzania Ltd Bw. Mark Mason akizugumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliandaliwa kwa ajili ya kuwapa taarifa juu ya maendeleo ya tumbaku na mambo mbali mbali wanayoyafanya katika kuisaidia jamii. Kampuni hiyo inafanya shughuli za Tumbaku huko Kinglowila, Morogoro.

Meneja Uhusiano wa Alliance One Tanzania Ltd, Bw. Hamis Liana akiwaeleza wahariri juu ya miradi mbali mbali ya kijamii inayotolewa na kampuni yao kupitia zao la tumbaku ambalo wanashughulikia huko mkoani Morogoro. Mkutano huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wahariri kutoka The African Bw. Shermax Ngahemera, Uhuru Bw. Damas na Bethuel Kinyori wa Corporate Digest na Meneja Uhusiano wa Silverbullet PR Nadine Kapya wakiwa katika mkutano na Alliance One Tanzania Ltd jijini Dar es Salaam.

Michuzi Jr

Kumbu Kumbu

BLOG MBALI MBALI

VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA HOUSE OF TALENTS

Computer Problems?

Clouds FM

BLOG IMETENGENEZWA NA:


·         Blogger news
·         Blogroll
·         About
·         Labels
·         . (1)
·         http://www.blogger.com/img/blank.gif (3)
Copyright © 2011 MICHUZI JR. All rights reserved.
Idadi ya watu
Jiachie Blog V2 | Modified by MKCT