Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aagiza Kampuni ya Ujenzi ya Electric International Company Limited Kukamilisha Ujenzi wa Skuli Mpya ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini iliyopo Paje Mtule Vinginevyo itafukuzwa na italazimika Kulipa Gharama Zote Zitakazojiri Kuitia Hasara Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua Jengo la Ofisi ya Elimu Wilaya ya Kusini liliopo Makunduchi likikaribia hatua ya uwezekaji ambapo aliahidi kuchangia Matofali 3000 na Mifuko ya Saruji 30 kukamilishia ujenzi huo.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Abdulla Mzee Abdulla akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini iliyopo Paje Mtule. Balozi Seif aliagiza kufutwa mara moja kwa mkataba wa ujenzi na kampuni ya Electric International endapo hatokamilisha ifikapo mwishoni mwa mwezi wa julai mwaka huu
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliangalia Darasa la Kompyuta la Charity School iliyopo Bwejuu baada ya kuweka jiwe la Msingi la Skuli hiyo.Kulia ya Balozi ni Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mh. Mohd Ibrahim, Naibu Waziri wa Elimu Mh. Zahara Hamad pamoja na Baadhi ya Waalimu wa Skuli hiyo ya Maandalizi na Msingi.