BREAKING NEWS: INTER MILAN YAMTIMUA RANIERI MASAA MACHACHE BAADA YA KUMWAMBIA KIBARUA CHAKE KIPO SALAMA.
Inter
Milan wamemtimua kocha Claudio Ranieri, katika siku ambayo Raisi wa
klabu hiyo Massimo Morratti alisema kocha huyo wa zamani wa Chelsea,
Valencia na Roma angekaa katika benchi la ufundi mpaka mwishoni mwa
msimu.
The
Nerazzurri walifungwa 2-0 na Juventus jumapili iliyopita, kuongeza
presha kwa Ranieri na kuchangia Moratti kutoa kauli ya: "Nafikiri
Ranieri atabakia mpaka mwishoni mwa msimu."
Lakini
la kushangaza masaa kadhaa baada ya kauli hiyo ya mwenye timu, klabu
ilitangaza kupitia mtandao wake kwamba Ranieri amefukuzwa kazi, hivyo
kumaanisha kwamba Milan sasa watakuwa wamefundishwa na makocha watatu
ndani ya msimu baada ya kumteua kocha wa timu ya vijana Andrea
Stramaccioni kubeba jahazi hadi mwishoni mwa msimu, akirithi nafasi
ambayo ilimshinda Gian Piero Gasparini na Ranieri.
Kocha
wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas anabakia kuwa mtu wakwanza
anayepewa nafasi ya kuchukua majukumu ya kuifundish klabu hiyo msimu
ujao.

0 Comments