Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, iliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2025 katika jiji la Windhoek.
Katika picha ya pamoja iliyopigwa mara baada ya tukio hilo la kihistoria, Dkt. Kikwete anaonekana katikati, huku pembeni kulia kwake akiwa ni mwenyeji wake – Rais mpya Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah.
Kushoto kwa Dkt. Kikwete ni Jenerali Epaphras Denga Ndaitwah, ambaye ni mume wa Rais mpya – akiweka historia kama “First Gentleman” wa kwanza katika historia ya Namibia.
Kushoto kwa picha hiyo ni Rais aliyemaliza muda wake, Mhe. Nangolo Mbumba, aliyehudhuria hafla hiyo na kukabidhi rasmi madaraka kwa mrithi wake. Kulia kabisa ni Mama Sustjie Mbumba, mke wa Rais Mstaafu wa Namibia.