Nahodha wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney, Jumatano ya August 23 2017 alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya England uamuzi ambao umekuja ikiwa ni siku 46 zimepita toka aondoke Man United na ajiunge na timu yake ya utoto ya Everton.
Wayne Rooney ambaye ametangaza kustaafu kuichezea England hadi anatangaza kustaafu August 23 2017, alikuwa kaichezea England michezo 119 na kufunga jumla ya magoli 53 toka alivyoitwa mara ya kwanza February 2003 England ilivyopoteza kwa magoli 3-1 dhidi ya Australia.
1- Rooney hadi anaondoka Man United na kurudi Everton bado anashikilia rekodi ya muda wote ya ufungaji bora wa ManUnited kwa muda wote kwa kufunga magoli 250 akivunja rekodi ya Sir Bobby Charlton.


2- February 2003 Rooney akiwa na miaka 17 na siku 111 anakuwa mchezaji mwenye umri mdogo kuwahi kuichezea England.
3- Kuwa mchezaji kijana mwenye umri mdogo kuwahi kusajiliwa Man United kwa dau la pound 30,000,000 akitokea Everton 2004.
4- Msimu wake wa kwanza akiwa Man United Wayne Rooney alifunga magoli 17 katika michezo 43 na kufanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo wa PFA na alifanikiwa kuchukua tena msimu unaofuatia.
5- Kufunga magoli 53 katika michezo 119 katika timu ya taifa ya England kunamfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa England.