Mamlaka katika Mji wa New Delhi, India zimearifu kuwa zimewakamata Wanawake wawili wa Kiafrika baada ya kuwakuta na Dawa za Kulevya aina ya cocaine yenye thamani ya Dollar Milioni 6 za Marekani.
Katika taarifa zilizochapishwa na DNA INDIA zimesema Narcotics Control Bureau (NCB) imemkamata mwanamke Mtanzania sanjari na Mnigeria wakati wanabadilishana dawa hizo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, Delhi Jumatano August 16, 2017.
Kwa mujibu wa Maafisa wa NCB, kufuatia upelelezi uliofanywa, walifanikiwa kumkamata Mtanzania huyo aliyetambulika kwa jina la Beatrice Kemmy Ndyetabula ambaye ana umri wa miaka 40, mara tu alipowasili kwa Ndege ya Go Air flight akitokea Mumbai.
Afisa Mkuu wa NCB alisema:”Alikuwa amebeba mabegi mawili. Ilikuwa wakati wa kukaguliwa ndipo zilibainika 4 kg za cocaine zikifungwa kwenye vifungashio 27. Alisema kwamba aliwasili Mumbai akitokea Kenya kisha akasafiri hadi Delhi kuukabidhi mzigo huo kwa muhusika.”
Maafisa hao walisema baada ya kumhoji, mwanaume ambaye alikuwa amkabidhi mzigo huo ambaye anafahamika kwa jina la Augustin, naye alikamatwa.
0 Comments