Related image
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo: DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,

Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 25 Agosti, 2017.

Tele Fax : 2153426


Tovuti : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananch wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya siku ya majeshi yanayoanza tarehe 25 Agosti 2017. Sherehe hizi ni za kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo hufanyika kila mwaka tarehe 01Septemba, mwaka huu sherehe hizo zitaadhimishwa wakati Jeshi linatimiza miaka 53 tangu lilipo asisiwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza Marehemu Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere Septemba Mosi 1964.
Mwaka huu 2017 maadhimisho hayo yatafanyika kwa wanajeshi kufanya shughuli mbalimbali kuanzia tarehe 25 Agosti 2017 hadi tarehe 31 Agosti 2017 na kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 01 Septemba 2017.Shughuli hizo ni pamoja na kufanya shughuli za huduma za kijamii katika maeneo jirani na vikosi vya Jeshi, Wanajeshi kuchangia damu salama katika hospitali mbalimbali nchini, kutoa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa Dar es salaam huduma za tiba zitatolewa katika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 2:00 asubuhi siku ya tarehe 01 Septemba, aidha wanajeshi watafanya michezo mbalimbali na wananchi Pamoja na kushiriki kufanya usafi kwenye maeneo ya kijamii (Hospitali, Masoko, Mashule n.k) na pia watafanya michezo Shirikishi na jamii inayowazunguka.

Kauli Mbiu ya maadhimisho haya ni Wiki ya Majeshi na Afya yako.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085