Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu.
MIAKA ya hivi karibuni mrembo ambaye ni kipenzi cha watu na Mshindi wa Shindano la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amekuwa kimya, hasikiki sana kwenye media tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Staa wa Filamu Bongo, Batuli.
Si mtu wa kuonekana viwanja tena hovyo, kujiachia na marafiki na hata ukitazama kwenye mitandao yake ya kijamii anachagua kwa sasa picha ipi ya kuposti ambapo picha anazoweka nyingi kwa sasa ni zile anazokuwa lokesheni ama kwenye shughuli maalum za kijamii na kwa uchache picha za baadhi ya washikaji zake.

Picha ambazo zinaonesha kukiuka maadili hatupii tena kama awali. Unaweza kusema pengine ni kwa sababu ameingia kwenye siasa ambapo miezi ya hivi karibuni alitangaza kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja.
Hata hivyo kitambo tu alikuwa anashiriki kwenye siasa lakini hakuwa mkimya kama ilivyo hivi sasa. Ukiachana na hayo, vipi kuhusu marafiki zake ‘wabeba mikoba?’ Wale aliokuwa anakula nao bata mpaka kuku wanaona wivu, wako wapi? Wamejichimbia chimbo gani kwa sasa?

Aunt Ezekiel.
Mbona hawaambatani naye na kuonekana naye kama ilivyokuwa awali? Ama nao wamepotea kwa sababu Wema amekuwa si mtu wa kiki kiivyo kwa sasa kutokana na kuishi maisha yenye ‘limit’? Ninapozungumzia wabeba mikoba wa Wema wengine wanaweza kuwa hawajawaelewa sawasawa. Wanaweza kujiuliza ni kina nani? Ngoja nikwambie; Baadhi yao ni kina Aunt Ezekiel, Jike Shupa, Muna, Kajala Masanja, Snura, Jack wa Chuz na Batuli. Hao walikuwa ni washikaji zake kwelikweli.

Kila kona Wema alipokuwa walikuwepo. Wengine walikula na kulala naye chumbani pamoja. Mfano Aunt Ezekiel. Kila mara alikuwa nyumbani kwa Wema na liliwahi kuibuka varangati kati ya Aunt na aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda, baada ya muigizaji huyo kulala nyumbani kwa Wema na Kadinda kumkuta. Kitendo hicho Kadinda alionekana kutokukifurahia akalianzisha vurumai na pia alikuwa akimshutumu Aunt kuwa ndiye chanzo cha ugomvi wa Wema na Kajala.