Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameelezwa kutoridhishwa na taratibu za uchunguzi na uendeshaji wa mashitaka ya rushwa zinavyochukua muda mrefu na ametoa wito kwa viongozi wa TAKUKURU kufanyia kazi eneo hilo ili vita dhidi ya rushwa ionekane ikizaa matunda haraka.

Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam akiwemo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.
Hata hivyo Rais Magufuli ameipongeza TAKUKURU kwa kazi wanayoifanya lakini huku akitaka juhudi ziongezwe zaidi ili watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa vya kutoa na kupokea rushwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.