Producer Daxo Chali kutoka Mj Records ametoa sababu za yeye kusimamia wasanii wa kike peke yake, na kuibua migogoro kwa jamii kuwa huenda producer huyo anajihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi na wasanii hao.
Daxo Chali amesema ameamua kuwasimamia wasanii hao kwa kuwa ameona fursa kwa wasanii wa kike, kwa kuwa wapo wachache kwenye game ya muziki hapa nyumbani.
"Tanzania kuna wasanii wengi wa kiume nikasema kama naanza kusimamia wasanii nitaanza na watoto wa kike kwanza kwa sababu wapo wachache nilete ushindani, nikatoa fursa nikamtoa Hytham, Hytham nilipomtoa alikuwa video vixen, baada ya hapo nikainsipire watoto wa kike wengi, na Mungu akijalia naweza nikachukua wasanii wa kiume pia", alisema Daxo Chali.
Daxo Chali aliendelea kusema kuwa kitendo hicho kinampa changamoto kubwa kwa kuwa inamlazimu kuwa karibu na wasanii hao, lakini hakuna mahusiano yoyote kati na wasanii ambao anawasimami kwa sasa, Hytham na Nini.
0 Comments