Director wa music video Bongo, Nisher amewataka mashabiki kupenda kujifunza historia za watu wenye mchango mkubwa katika ukuajia wa tasnia ya muziki na video production.
Akijibu maswali ambayo alikuwa akiulizwa na mashabiki wake katika mitandao ya kijamii, Nisher ameeleza kuwa hiyo itasaidia kuheshimu kazi ambayo ilishakwisha fanyika hapo awali.
“Kwa mfano watoto wa sasa hivi wanaweza wakaamka wakashika simu zao, hawaangalii historia wao wanaangalia kuna director mpya anaitwa ‘Dumu’, ni safi sana ndio anaongoza sasa hivi, ndio ana-trend. Someni historia huyo director Dumu amepata inspiration kutoka kwa nani?” amehoji na kuongeza.
“Zamani kulikuwa na watu kama wakina Nisher na mpaka sasa hivi wapo, AJ, John Kallage, wakina Karabani watu ambao wameshiriki katika kukuza industry mnajifunza hiyo?” amesema.
Nisher amesema faida ya kujifunza hayo ni kuelewa kuwa watu hao wamekutana na changamoto gani na wakati gani ulikuwa mwepesi kwao na wakati gani ulikuwa mgumu kwao.
“Kwa mfano kabla ya Diamond kulikuwa na watu kama Dully Sykes, kabla ya Vanessa Mdee kulikuwa na watu kama Ray C, Lady Jaydee je mnachukua muda wa kujifunza kwa watu kama hao?. Ni rahisi kumnyooshea kidole Lady Jaydee amefeli, hapana, amefungua milango kibao,” amesisitiza.