Image result for nec tanzania
Kwa Mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika leotarehe 21 Agosti, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kumi na wawili (12) kujaza nafasi wazi za Madiwani katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara.
Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
NA.
JINA
CHAMA
HALMASHAURI
  1. 1
Ndugu Saida Idrisa Kiliula
CUF
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  1.  
Ndugu Sophia Charokiwa Msangi
CCM
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  1.  
Ndugu Shahara Selemani Nduvaruva
CCM
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  1.  
Ndugu Neema K. Nyangalilo
CCM
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

  1.  
Ndugu Farida Zaharani Mohamed
CCM
Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  1.  
Ndugu Lucia Silanda Kadimu
CCM
Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)

  1.  
Ndugu Amina Ramshi Mbaira
CCM
Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  1.  
Ndugu Janeth John Kaaya
CHADEMA
Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  1.  
Ndugu Sara Abdallah Katanga
CHADEMA
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

  1.  
Ndugu Ikunda Massawe
CHADEMA
Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  1.  
Ndugu Tumaini Wilson Masaki
CHADEMA
Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  1.  
Ndugu Elizaberth Andrea Bayyo
CHADEMA
Halmashauri ya Mji wa Mbulu

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi.
 Imetolewa leo tarehe 21 Agosti, 2017
Kailima, R. K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI