Staa wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda aliyewahi kupata umaarufu mkubwa akiwa kwenye mahusiano na Shilole ametoa malalamiko yake Instagram kuhusu kuumizwa kila anapokuwa kwenye mahusiano.
Kwenye IG Yake Nuh Mziwanda ameandika ” Nimejifunza mengi sana kwenye life style yangu ya kimapenzi na najitoaga sana ila siku ya mwisho naumizwa ‘je unahisi Mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu nae?Leo Nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili “
Hivi karibuni Ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal ilivunjika ikiwa ni mwaka mmoja tu umepita, Nuh na Nawal wana mtoto mmoja wa kike anaitwa Anya.