Muigizaji na mnenguaji  Husna Sajent ameibuka na kumsifia mpenzi wake ambaye ni msanii wa singeli Tanzania Dullah Makabila na kusema ni mwanaume anayewajali watoto wake sana kuliko hata wazazi wenzake alioza nao ambao pia ni watu maarufu.
Sajent amesema pamoja na kwamba ameingia kwenye mahusiano na msanii huyo akiwa tayari ana watoto wawili ambao mmoja alimpata akiwa na muigizaji Gabo, na mwingine amempata na muimbaji Charles Baba lakini Makabila amekuwa akiwaonyesha watoto wake mapenzi mazito kuliko baba zao.
"Nachopenda ni kwamba Dullah anawapenda sana watoto wangu kuliko hata hao baba zao maana yupo nao 'busy' sana. Kusema kwamba wazazi wenzangu watahitaji watoto wao hawawezi kwa sababu wao wana familia zao tayari na mimi nina maisha yangu. Wakati mwingine huwa nawauliza au wake zao wanawazuia au maana wanatambua kuwa wana watoto lakini hawajali kibile wakati mimi nimewapa uhuru wanangu kuwa karibu na baba zao lakini wao hawaonyeshi kujali kiivyo, lakini kwa vile wanangu wanasoma shule nzuri na waishi vizuri mengine mimi sijali"Sajent alifunguka.
Pamoja na hayo Sajent amesema kwa jinsi wanavyoishi kwenye mahusiano na Dullah Makabila anaamini ndoa ipo mbeleni ingawa hapendi kuzungumzia sana suala hilo na kwamba anamuachia majukumu mshenga pamoja na mpenzi wake huyo.
"Nataka watanzania wafahamu kuwa mimi na Dulla kabila ni wapenzi wa muda mrefu sasa na tupo katika hatua za mwisho kufuatilia maswala ya kufunga ndoa japo mimi kama mwanamke siwezi kuongelea swala la ndoa sana namuachia Dulla" Sajenti
Pia  Husna aliendelea kusema kuwa anaamini mahusiano yake na Dulla yatadumu kwa muda mrefu tofauti na watu wengine maarufu kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa wakiheshimiana na kuwekana wazi matatizo yao pale inapohitajika kwa kuwa wanaaminiana.