Aliyekuwa meneja wa msanii Ommy Dimpoz, Mubenga amesema ameamua kuachana na yale yote yaliyotokea kati yake na msanii huyo ili maisha mengine yaweze kuendelea.
Meneja huyo ameeleza kuwa kwanza si kweli Ommy Dimpoz alimfukuza kama inavyosemekana kwani Dimpoz alifika kwake akiwa hana kitu chochote.
“Hakuja na mtaji kusema nataka unifanyie kazi yangu, mimi ndiye nilitafuta kila kitu, nilimpigania mtaani kupata pesa ya kuweka kwenye muziki wake, radio zote nimemtambulisha mimi, hakuna sehemu ambayo Omary alinipeleka,” alisema
“Baada ya kutoka unajua tena vijana wanabadilika ndio akaanza hizo, mimi nimemuachia Mwenyenzi Mungu, nimemuacha apambane na hali yake,” amesisitiza.
Pia meneja huyo aliendelea kusema yeye ndiye alimtoa Ommy Dimpoz mtaani na kumpeleka Kinondoni na kumpa backup kutoka kwa watu wake wa karibu na kila kitu kilikuwa juu yake ila sasa ameamua kuachana na hayo yote.
0 Comments