Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akiwashukuru washiriki wa mkutano huo wakati wa Utambulisho kwenye ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini.# Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Mkutano huo wa 37  wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit),unawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt John Pombe Magufuli.Katika mkutano huo Tanzania itakabidhi nafasi ya  Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.