KESI inayomkabili Mshtakiwa  Salum Njwete (Scorpion), ya kuiba , kumjeruhi  na  kumtoboa macho Saidi Mrisho leo imehairishwa kwa mara nyingine  Mahakama ya Wilaya ya Ilala.Shauri hilo  ambalo limehairishwa na Mwendesha mashtaka wa Serikali Salum Katuga  mbele ya Hakimu Adelf Sachore, ambapo alidai  walikuwa wamejiandaa kuendelea na kesi lakini Hakimu anaendesha  kesi hii amepata udhuru."Muheshimiwa Shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na upande wa jamhuri tulijiandaa na shahidi mmoja lakini bado yupo kwenye  daharula tunaomba Mahakama yako itupangie tarehe nyingine" alisema KatugaKwa upande wa Wakili wa utetezi wa Mshtakiwa Juma Nassoro alipoulizwa kama anakubaliana na udhuru huo alikubali kwa kusema sawa na wapangiwe tarehe nyingine.
Hakimu alisema kesi hiyo italetwa tena Agusti  28 Mwaka huu, Mshtakiwa amerudishwa rumande.