Siku moja baada ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuchezesha droo ya kupanga makundi ya UEFA Champions League mjini Monaco Ufaransa, leo August 25 2017 imechezeshwa droo na kupangwa makundi ya michuano ya UEFA Europa League.

Droo imechezeshwa lakini imeambatana na utolewaji wa tuzo ya mchezaji bora wa UEFA Europa League msimu wa 2016/2017 ambapo staa wa Man United Paul Pogba ameshinda tuzo hiyo kwa kupata point nyingi zaidi, Pogba aliisaidia pia Man United kutwaa taji la Europa.
Rais wa UEFA Aleksander ÄŒeferin akimkabidhi Paul Pogba tuzo
Leo sio siku nzuri kwa mashabiki wa Arsenal ambapo wameishuhudia timu yao ya Arsenal ikipangwa kwa mara ya kwanza katika makundi ya UEFA Europa League, baada ya zaidi ya miaka 20 kupita hivyo Real Madrid na FC Bayern Munich ndio zinabaki kuwa timu pekee ambazo hazijawahi kukosa kushiriki Champions League kwa miaka 20 iliyopita.
Makundi ya UEFA Europa League msimu 2017/2018