Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati akisindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa Kulia yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini hapo Zanzibar Ocean View.

Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini wa Kampuni ya { SRT } kutoka
Nchini Uingereza Bwana Simon Tucker akielezea umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya Baharini hapa Zanzibar.

Wa Pili kutoka Kulia waliokaa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa na wa kwanza kulia ni Bwana Lazaria Moh'd Said