Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa.

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,Machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa
Waziri Mkuu, MizengoPinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Japan, Bw. Masahito Kawashima kabla ya kuzungumza na ujumbe wa wawekezaji wa Kijapan kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo Machi 17, 2015.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Japan baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwasili kwenye ubalozi huo Machi 17, 2015 kuzungumza na watanzania waishio japan.
Waziri mkuu, Mizengo Pinda na mkewe wakitia saini kitabu cha wakgeni kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo nchini Japanbaada ya kuwasili ubalozini hapo kuzungumza na Watanzania waishio Japan Machi 17, 2015. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza muda wake, Salome Sijaona na Wapili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Batilda Buriani na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mahadh Maalim.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto, Petro Mosongo (kulia), Neema Mosongo (wapili kulia) na Stacey Kambona baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Tokyo kuzungumza na watanzania waishio Japan Machi 17, 2015.
Waziri mkuu, MIzengo Pinda akizungumza na balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona (katikati) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed (kulia ) kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Japan baada ya kuzungumza n a watanzania waishio Japan Machi 17, 2015. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan, David Semiono.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa Kati picha ya pamoja na watanzania wanaosoma nchini Japan baada ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo ulioko Tokyo Machi 17, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)








0 Comments