Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ally Idd akisalimiana na wasanii wakati akiwasili katika uwanja wa Amani Zanzibar kw ajili ya ufunguzi wa Tamasha la wasanii la kuimarisha uzalendo Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif ally Idd akizungumza katika tamasha la wasanii ambapo aliwataka kutumia karama zao kuhamasisha uzalendo kwa watanzania hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya pia kutumia nafasi yao katika jamii kuelimisha jamii kuisoma na kuielewa Katiba Inayopendekezwa ili kuona ni jinsi gani imegusa maisha ya watanzania ili waweze kufanya uamuzi sahihi wakati wa kupiga kura ya maoni.
Msanii wa kizazi kipya nchini Nickson Simon a.k.a Nikki wa pili akizungumza kwa niaba ya wasanii na kueleza ni jinsi gani haki za wasanii zimetambuliwa kwa mara ya kwanza katika Katiba Inayopendekezwa, wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif ally Idd.
Msanii wa Kizazi kipya kutoka Zanzibar Jamila Abdallah (Baby J) akitumbuiza wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
‘Zuwena Mohamed A.KA. Shilole akitumbuiza wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
Nikki wa pili akipagawisha maelfu ya mashabiki waliohudhuria Tamasha hilo.
Wasanii wa kundi la Navy Kenzo wakiwa jukwaani wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
Vijana waliohudhuria tamasha hilo wakisoma Kijarida cha maudhui ya Katiba Inayopendekezwa kilichoandaliwa kwa lugha nyepesi wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Watanzania wameaswa kuisoma ili waweze kuielewa Katiba Inayopendekezwa na kufanya uamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura ya maoni.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Idd wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar Machi 7, 2015
Balozi Seif alisema kuwa huu ni wakati wa Watanzania kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kuona ni jinsi gani haki za makundi mbali mbali katika jamii zilivyoainishwa na namna watakavyonufaika
“natoa wito muisome Katiba Inayopendekezwa ili kuona jinsi haki za makundi mbalimbali katika jamii zilivyoanishwa na muweze kutumia fursa hiyo kufanya maamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura ya maoni wakati utakapofika” Alisema Balozi Seif.
Aidha Balozi Seif alisema kuwa huu ni wakati wa wasanii kutumia nafasi yao katika jamii kuelimisha juu ya maudhui ya Katiba Inayopendekezwa kwa kutumia kazi zao za sanaa.
Akiongea kwa niaba ya wasanii katika Tamasha hilo msanii wa kizazi kipya Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili alisema kuwa wasanii wamefarijika sana hasa baada ya Katiba Inayopendekezwa kutambua haki za wasanii kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.
Nickson aliongeza kuwa walianza mchakato wa kupigania haki za wasanii kwa kutoa maoni wakati wa Tume ya warioba lakini hazikuingizwa katika Rasimu iliyotolewa na tume hiyo hivyo kuwabidi kupeleka maoni yao kwenye Bunge Maalum la Katiba na hatimaye zimejumuishwa ndani ya Katiba Inayopendekezwa.
“Baada ya haki za wasanii kutokuwepo kwenye Rasimu ya Katiba iliyotolewa na tume ya Jaji warioba wasanii tuliamua kwenda kupeleka maoni yetu kwa mara nyingine kwa mwenyekiti wa Bunge Maalum na baada ya kutoka kwa Katiba hii Inayopendekezwa haki za wasanii zimeweza kutambulika”. Alisema Nickson.
Tamasha hilo linadhumuni la kuhamaisha uzalendo kwa watanzania hasa kwenye masuala ya kitaifa ikiwemo mchakato wa upatinaji wa Katiba Mpya na uchaguzi Mkuu

0 Comments