Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu hoja mbali mbali zilizoletwa na kamati ya soko la  Kilombero ikiwa pamoja na kupandishiwa kodi bila utaratibu maalum.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Arusha kwenye soko la Kilombero ambapo walisalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi.
 Wananchi na Wafanyabiashara mbalimbali katiko soko la Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao ikiwemo pia na kuyasikiliza matatizo mbalimbali yanawakabili katika soko hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali wakila chakula kwa Mama Lishe wa soko la Kilombero,jijini Arusha,pichani kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Vijana,Mh.Catherine Magige.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakinywa kahawa mara baada ya kumaliza kuwasalimu na kuzindua shina la wakereketwa wajasiriamali Oysterbay, Unga ltd, Arusha.

Ameongeza kuwa CCM ni chama kinachotakiwa kuwasemea na kuwatetea wanyonge na siyo kuwakandamiza na kuwaonea  “Lazima viongozi na watendaji wa serikali na chama wawajibike kwa wananchi ambao ndiyo walioingia mkataba na CCM ambayo iliunda serikali inayotekeleza ilani yake” amesema .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Arusha akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inayotekelezwa na serikali ya CCM huku akihimiza uhai wa Chama hicho akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wengine wa CCM kuelekea kwenye soko la Kilombero,jijini Arusha,kusikiliza kero na matatizo mbalimbali yaliyopo ndani ya soko hilo.