Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.) (wa pili kushoto mstari wa mbele) akishiriki matembezi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu ya Kanisa Katoliki Sinza, Dar es Salaam mapema leo asubuhi..Wa kwanza kushoto ni Paroko, Father Cuthbert Maganga Sasagu, na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Bw. Arnold Mwasumbi. 
Matembezi ya hisani yaliyoanzia Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge yakielekea Parokia ya Sinza kupitia barabara ya Shekilango. Matembezi hayo ya kilomita mbili yaliongozwa na Mhe. Membe. 
Waziri Membe akizungumza na waamini wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu Sinza (hawapo pichani) 
Baadhi ya waamini wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu Sinza wakimsikiliza Waziri Membe 
Waziri Membe akiendelea kuzungumza na waamini wa parokia hiyo. 
Waziri Membe akipokea Zawadi ya picha kutoka kwa Paroko Sasagu 
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongowa wa parokia ya Sinza. 
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na wapuliza Tarumbeta