Baba mzazi wa marehemu Focus Saimon (9).Focus aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, amedaiwa kufanya tukio hilo Jumamosi iliyopita kwa kufunga gauni la mdogo wake shingoni na kujitundika kwenye komeo hilo mpaka kukata roho.
Katika hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda, Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa sebule yao.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa siku ya tukio, Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo wake, Irene Steve (5).
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.
Mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria (kushoto) akiwa na mama mzazi wa Focus Saimoni.“Nilimwambia Focus usinitanie mbona hauzungumzi na mimi, nilipomwangalia vizuri ndipo nikaona ana damu mdomoni, nikakimbia kwa mama mdogo anayeishi jirani na kumueleza,’’ alisema Irene.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria alisema naye hakuamini tukio hilo.“Aliponiambia Focus kaning’inia mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.“Ila mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.
Mdogo wa marehemu Focus Saimoni, Irene.
Akizidi kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema alishangaa wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi aliukuta mwili umeshushwa chini. “Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna aliyenijibu,’’ alisema Catherine.Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.
0 Comments