
Mtawa Cristina lishinda shindnao la Voise makala yaliyofanyw Italia mwaka jana
Mwimbaji mtawa aliyeshinda tuzo la The voice la Italia atoa wimbo mpya unaofanana na ule wa mwimbaji mtajika wa Marekani Madonna kwa jina 'Like a Virgin'.Mtawa Cristina Scuccia, ambaye alishinda katika mashindano ya uimbaji hapo juni amesema alijichagulia wimbo huo mwenyewe " bila nia ya kuzua gumzo ama kushangaza", lakini amesema pia yuko tayari kukosolewa.
"Ni wimbo unaohusu uwezo wa upendo wa kuwabadilisha watu kuwa wapya. Kuwakomboa kutoka kwa yaliyopita. Na hivyo ndivyo nilivyotaka kuutafsiri," aliliambia gazeti moja la kikatoliki la Avvenire.

Cristina na tuzo la Voice nchini Italia
Bali na kuiga wimbo huo wa aina ya muziki wa pop, mtawa huyo mwenye umri wa miaka 26 ameubadilisha wimbo huo kuwa wimbopendwa wa masimulizi.
Ingawa katika video ya Madonna ya wimbo huo, Madonna huonekana akinengua mauno kwa njia ya kuvutia hisia akiwa katika dau mmoja huku akifuatwa na Simba katika eneo la Venetian huko Las vegas, mtawa huyo ameamua video yake kuwa tulivu na yenye heshima.
Mtawa Cristina anasema hana uhakika kama Madonna amesikia habari hizi kuhusu mabadiliko yaliyofanyiwa wimbo wake. "Lakini ningependa sana kuona uso wake wakati anapopata habari hizi, na wakati anapofichuliwa kwamba ni mtawa anayeimba."
0 Comments