.jpg)
Barua yangu kwa vijana, mambo yamebadilika sana siku hizi,mazuri yaonekana mabaya na mabaya ndio mazuri mbele za watu, ukiangalia kizazi chetu hichi utagundua kwamba ni kizazi kinachokumbwa na mambo mengi sana na haijawai tokea. Kwanini vijana?
Tumependa starehe za dunia bila kua na busara ya nini cha kufanya na kwa mda gani wa kufanya.tumejiingiza katika mambo yasiofaa kwa tamaa ya pesa. Magonjwa yanatumaliza vijana jamani tubadilike na tupende uhai wetu kuliko kitu chochote.hata kama hali mbaya.huwezi kuibadilisha ukiwa kaburini. Ukimwi unatumaliza kila kukicha,vijana tuamke. Serikali inajitahidi lakini pia ni uwajibu wetu kujilinda.
Kuna wengi wanaopotea kila siku lakini chakusikitisha ni kwamba asilimia 67 ni vijana na sio wazee, kwanini mambo yamebadilika kiasi hicho?ni kwasababu tumekua na tamaa ya mafanikio kuliko kupenda uhai wetu. Tunapenda kutamaani wengine waliofanikiwa bila kujiuliza
Mapito yao kabla ya mafanikio yalikua vipi na kwasababu ya kuto kujua
Tumejikuta tukifanya maamuzi ya msingi bila kufikilia.
Napenda kuzungumza na vijana wanaofikili kwamba kua na wanawake
Wengi ni sifa ama kitu cha heshima kwamba kua na mwanamke moja
Ndio ishara ya utu uzima maana jamii itakueshimu kama umetulia na
Sio vinginevyo,pia napenda kuongea na vijana ambao wanapenda
Kuiga wengine na starehe za kila siku kwamba panga pia mda
Kufikilia maendeleo yako mwenyewe.Tanzania ilipofikia inaitaji mchango wako kama kijana.
kwa mawasiliano
0688 440029
instagram; ELLYDAVID1
0 Comments