.jpg)
Unaweza ukawa wewe ni mtu wa kuongea mengi na watu wakakupenda kwakua unajua kuongea lakini mwisho wa siku watu watasahau maneno ya na kukumbuka matendo yako. Nilivyokua nakua, nilikua ni motto mtundu na kila nilichokua nashika na mikono yangu lazima kiaribike, siku moja bibi aliniuliza swali ambalo kwa kipindi nilichoanza kukua lilileta maana. Aliniuliza. Utakumbukwa kwa lipi?
Kila mtu anaweza kuongea lakini sio wote wanaweza kutenda. Hivyo matendo yetu yanabaki kua kumbukumbu katika maisha ya watu kuliko maneno.
Swali ni, Ni matendo gani utakayo kumbukwa nayo? Siku moja nilienda kutembea bagamoyo na kujifunza kuhusu historian a mambo yaliotokea hapo zamani.
Tulikutana na makaburi ambayo kaburi moja lilikua na moja wa wazungu aliejiua kwa wivu wa mapenzi.kilikua ni kitu cha kushangaza lakini baadae nilielewa.
Matendo yetu ndio yanayojenga eshima yetu ama kutupa cheo katika myoyo ya wengi. Kuna watu ambao kwa muonekano wanaonekana vizuri lakini wakipita sehem watu hukasilika ama huchukizwa nao nah ii ni kwasababu ya vitu walivyofanya. Matendo yetu yanaweza kujenga ama kubomoa watu.
Na ni rahisi watu kusamee ulichokisema kuliko ulichokitenda ,hivyo bado hujachelewa kubadilisha njia zako. Na haijalishi umetenda maovu kiasi gani, lakini unaweza kubadilika na kuanza kutenda mema, ni rahisi kubadilisha mawazo ya watu. Kwasababu watu wanaamini wanachokiona kuliko walichosikia.
Kuna rafiki yangu mkenya ambae nimemjua kwa kipindi kirefu,lakini alikua ni mtu asie na heshima kwa baba yake. Kila alivyotumwa aligoma na kuona amekua na alipenda sana kujibishana na baba yake,watu walimshauri lakini hakuonesha mabadiliko. Ilifika siku,Mungu akamchukua baba yake. Na tulivyoenda kwenye mazishi kijana Yule alionesha kusikitika kwa hali ya juu na baada ya mazishi, alitoa pesa ya kupendezesha kaburi la baba yake. Nilianza kusikia watu wakiongea mengi ambayo sio ya kufuraisha juu ya huyo kijana,lakini nachojaribu kusema.
Tenda mema kutoka moyoni ili watu waone mabadiliko yako kwasababu huwezi ukajifanya umebadilika na tabia ya mtu haifichiki milele ipo siku itatoka na kuonekana mbele za watu.
usisite kuwasiliana nasi
mawasiliano
0688440029
0 Comments