.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*)
Habari zenu watanzania wenzangu,natumaini wote ni wazima na wenye afya na aman.nimerudi ili tuweze kuzungumzia kujifunza.ninavyo ongelea kuhusu kujifunza siongelei kwenda tu darasana na kupata elimu bali kujifunza kwa wale waliokupita uwezo wa kufikili na pia kimaendeleo. Tatizo letu hapa kwetu ni kwamba mtu anapojitokeza kua zaidi yaw engine badala ya kujifunza kutoka kwake,tutajaribu kumshusha na kumrudisha nyuma kimaendeleo.kama tutakua na moyo kama huu hatutajua uzuri utokao kwa wengine na juhudi zao.tunaishi katika nchi ambayo watu hufanya vitu kwa siri kwa kuhofia kupatwa na mabaya ambayo yanasababishwa na wengine.kwanini tuendelee kuishi hivyo nawakati tunaweza leta maendeleo kati yetu wenyewe na nchi yetu pia? Kuna nchi za wenzetu,wakiona mtu ana upewo tofauti basi wataungana kumsaidia kimawazo,kifedha na pia kimaendeleo. Watanzania tuna uwezo na ukarimu wetu uwe ukamilifu wetu hata kwa wale waliotuzunguka.tukubali kujifunza.
Kwa wanafunzi wanaosoma chuo na sekondari, kibuli ni kabuli. Na kamwe unapokua na kibuli huwezi kujua zaidi ya unachojua. Haupungukiwi chochote kwa kua mnyenyekevu kwa wale waliokuzidi kwasababu hakuna mtu ataekubali kukupa siri ya mafanikio yake ukiwa na tabia mbaya (attitude)
Na pia kumcha Mungu ni jambo la msingi kwasababu kuna vitu hatuwezi kwa uwezo wetu wenyewe,hivyo katika kila jambo tunaitaji kumshirikisha Mungu atusaidie pia na atupe muongozo katika maisha yetu. Tusambaze upendo.tuonane tena wiki ijayo.nawatakia wikendi njema.
Kwa mawasiliano
0688440029
instagram; ellydavid1
0 Comments