Takribani wiki sasa kumekuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu hayuko sawa katika mahusiano yake ya kimapenzi na nguli wa Bongo Fleva, Diamond Plutnumz….
Rafiki huyo amedai kuwa mara kwa mara Wema amekuwa akijiuliza sababu ya kuandikwa taarifa mbalimbali zisizo na kichwa wala miguu ambapo mwisho wa yote hupata jibu ni kwa sababu ya kuwa na mahusiano na Diamond…
“Wakati mwingine anasema angelijua bora angebaki bachela kwani kuna kikundi cha watu hakipendi kumuona akiwa na Diamond hivyo kinafanya kazi ya kumzushia taarifa zisizoeleweka kila mara kwa lengo la kumshushia hadhi,” kimesema chanzo hicho.Mwandishi alipokiuliza chanzo hicho ni kwa kiasi gani Wema anamwamini Diamond kilisema:
“Ukweli
ni kwamba Wema anampenda sana Diamond lakini hamwamini kwa
sababu wakati mwingine taarifa zinazoandikwa magazeti hutolewa
na Diamond mwenyewe, hali hiyo inampa wakati mgumu sana Wema
kujua ashike wapi na wapi apaache,”
“Unajua Diamond haaminiki, unaweza kukuta Wema anagombana na watu kumbe mtoa taarifa ni Diamond mwenyewe.”


1 Comments