Asanteni sana vijana wenzangu kwa kusoma na kufatilia makala hizi za kujengaNa kuelimisha.ni maombi yangu kwa Mungu kwamba makala hizi zitaendelea kuajengaZaidi.katika maisha yetu kama vijana,kuna vitu vingi vijavyojitokeza hasa pale tunapoanzaKukua.lakini katika yote, sio yote ni yetu,mengine ni kama mitego ama vizuizi vya kutuzuia
Tusifike mbali.katika vitu vinavyotuponza sisi vijana ni tamaa ya kutaka kua kama wengineNa pia kupenda kujulikana na mengine mengi ambao sitayataja kwa leo. Sababu kuuAmbayo inatufanya tusiendelee kama vijana ni kwamba tunapenda kutangulia kufanya

Vitu vya muhimu kuliko vya msingi maishani mwetu.kwa mfano. Nilipokua shule kuna kipindi
Nilipewa ada ya shule lakini nikaamua ninunue simu mpya,simu ni nzuri na muhimu kwaajili ya
Mawasiliano lakini sio cha msingi kwa wakati huo.nilijikuta nikitumia ada ya shule ambayo mpaka
Leo wazazi wangu hawakujua kwasababu sikufanya mitiani na nikaamua kunyamaza.
Katika maisha yetu,sio kila kitu ni kwaajili yetu hata kama vinavutia katika macho yetu.
Jambo lolote la msingi litajenga maisha yako lakini la muhimu litakufuraisha kwa mda.
Tunaitaji hekima ya kujua lipi la kufanya na lipi la kulikumbuka baadae kwasababu kila
Kosa tunalofanya wakati wa kujenga msingi wa maisha yetu litakuja kuonekana mbele
Ya safari.tuonane tena siku nyingine.naomba mtembeleeni facebook page yangu na pia
Instagram kwa wale ambao mpo.asanteni sana.

Mawasiliano
Facebook page; Elly david Tanzania
Instagram  ;  ellydavid1