.jpg)
Nipende kuwashukulu vijana wenzangu na hasa kwa wale wanaopenda kusoma makala zangu.Tuzidi kuombeana uhai.leo napenda kuongelea kuhusu swala la kujishugulisha ambalo wengiLimekuwa likiwasumbua sana hasa kwa sisi vijana.nimekutana na vijana wengi ambao wamemalizaMasomo yao wakiwa na matumaini ya kupata kazi kubwa na kukaa maofisini lakini kwa bahatiMbaya wakawa bado hawajapata kazi na kuhisi labda wana tatizo lolote.ni kawaida kwa mambo kamaHayo kutokea kwasababu kwa sasaivi kila mtu anatafuta kazi na wengi hupenda kazi zenye mishahala
Mikubwa. Tunaishi katika kipindi ambacho mashindano na ubinafsi umekua wa kasi sana kwasababu
Wengi huwapa kazi ndugu jamaa na marafiki hata kama hawana vigezo vya kutosha na
Ndio maana utaenda ofisi nyingine ukakuta ni kubwa na zenye muonekano mzuri lakini hawana huduma
Bora zenye kuridhisha.hivyo huku ukisubili kuna vitu ambavyo unaweza ukajituma ili uweze kujiingizia
Kipato hata kama kitakuwa kidogo lakini ni bora kua na hicho kuliko kukosa kabisa.
Hivyo napenda kuwashauri vijana wenzangu ambao memaliza masomo na umekua ukitafuta kazi kwa
Mda mrefu kwamba unaweza ukajishugulisha na kitu chochote chema na chenye maendeleo huku
Ukisubilia bahati yako ya kupata kazi. Usivunjike moyo kwasababu hujapata na kila wakati unapopata
Wazo la kukata tama mshukulu Mungu kwakua kuna wale ambao hawakupata uwezo wa kwenda hata
Darasanai. Tukutane tena katika makala yetu ijayo.
0 Comments