Award: James Rodriguez's six goals were enough to make him the first Colombian to win the Golden Boot
Tuzo: James Rodriguez amekuwa mchezaji wa kwanza wa Colombia kushinda kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao sita.

NYOTA mpya wa Real Madrid,  James Rodriguez amesema kushinda kiatu cha dhahabu katika fainali za kombe la dunia ilikuwa ndoto iliyotimia.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 aliposti picha katika mtandao wa Twita akiwa na tuzo ya kiatu cha dhahabu aliyoshinda baada ya kufunga mabao sita katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Ili kushangilia tuzo hiyo, nyota huyo wa Colombia atacheza msimu ujao kwa kutumia viatu vya dhahabu na anatarajia kuongeza mabao mengi zaidi.
"Nilikuwa na matumaini ya kushinda kwasababu mara zote nilikuwa naota kushinda kitu kama hiki,' James aliwaambia waandishi. 'Hii pia ni chanzo cha furaha kwa nchi yangu ya Colombia. Kwasababu walinipa nguvu sana, kwahiyo nilitakiwa kushinda tuzo.'
New boots: The Colombian midfielder will play in new golden boots this season to celebrate his achievement
Viatu vipya: Kiungo huyu wa Colombia atachezea viatu vya dhahabu msimu ujao kama sehemu ya kusherehekea mafanikio.

MABAO YA RODRIGUEZ KOMBE LA DUNIA 2014 


  • Alifunga moja, na kutengeneza moja dhidi ya Ugiriki.

  • Alifunga moja, na kutengeneza moja dhidi ya Cameroon

  • Alifunga bao zuri dhidi ya Japan

  • Alifunga mabao mawili dhidi ya Uruguay, likiwemo bao la mashindano 

  • Alifunga penati Colombia wakifungwa  2-1 na Brazil katika mchezo wa robo fainali.
  • chanzo:mpenja