Dereva ambaye alikuwa akiendesha basi linalowabeba wachezaji wa Yanga, Maulid Kiula, amefariki dunia.
Kiula amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa siku kadhaa na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amethibitisha hilo.
Bado haijaelezwa mipango ya mazishi, lakini mashabiki wanaweza kumkumbuka zaidi kupitia tukio la yeye kujeruhiwa wakati mashabiki walipolishambulia basi la Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara.
Mungu aipumzishe roho ya mwanamichezo huyo.
AMINA.

0 Comments