KIPA Pepe Reina amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 2 kutoka Liverpool kwenda Bayern Munich.
Kipa huyo wa Hispania, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Napoli, amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na mabingwa hao wa Ujerumani.
Anatarajiwa kuwa msaidizi wa kipa wa kwanza wa mabingwa hao wa zamani wa Ulaya, Manuel Neuer Uwanja wa Allianz Arena msimu ujao. 

Dili limetiki: Kipa Pepe Reina akiwa amepozi na jezi ya timu yake mpya, Bayern Munich baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu
0 Comments