412895_heroaKOCHA mkuu wa Nigeria, Stephen Keshi ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

Mabingwa hao wa soka barani Afrika wanaenda kushiriki fainaili hizo kwa mara ya tano na wamepangwa kundi moja na Argentina, Iran na Bosnia.
 
Wachezaji wazoefu kama Vincent Enyeama, Austin Ejide, Joseph Yobo  na Elderson Echiejile  waliokuwa sehemu ya kikosi cha fainali za mwaka 2010 nchini Afrika kusini wamejumuishwa katika orodha hiyo ya mwisho.
Mfungaji bora wa fainali za 29 za AFCON, Emmanuel Emenike, Godfrey Oboabona, John Obi Mikel na Victor Moses wanatarajia kucheza fainali zao za kwanza za kombe la dunia.
Kusoma Kikosi kizima bofya www.bkmtata.blogspot.com