Maafisa wa Qatari watahojiwa leo na mchunguzi wa Fifa Michael Garcia kuhusu madai juu ya rushwa iliyotawala wakati wa utoaji wa zabuni ya Kombe la Dunia mwaka 2022.
The Sunday Times lilieleza kwamba Mohamed bin Hammam, makamu wa rais wa zamani wa fifa, alifanya malipo ya jumla ya dola 5m (paundi 3m) kwa maafisa wa soka ikiwa ni kurudisha shukrani kwa kuipatia zabuni ya kuandaa Kombe la Dunia Qatar mwaka 2022.
Kamati ya zabuni ya Qatari inakanusha madai na kusisitiza Bin Hammam hakufanya hivyo kwa niaba ya Qatar.
Garcia, wakili wa Marekani, alitangaza mapema wiki hii kwamba uchunguzi wake katika mchakato wa zabuni kwa fainali zote za 2018 na 2022 za Kombe la Dunia na atahitimisha Juni 9.
Amesema atatoa taarifa yake ya mwisho kwa Kamati huru ya Fifa, wiki sita baadaye.
The Sunday Times linadai kwamba Bin Hammam, ambaye anatokea nchini Qatar, alitumia dola 5m kununua sapoti kwa maafisa wa soka ili kuipatia nchi yake zabuni ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2022.
Vyanzo kutoka Fifa vinasisitiza Garcia alikuwa tayari makini juu ya madai hayo kufuatia uchunguzi wa awali dhidi ya Bin Hammam ambaye ni kiongozi wa Asian Football Confederation.
Kamati hiyo ya Qatar ilisema kwamba itashirikiana na Garcia katika jambo hili ikiongeza: "Tutafanya kila kile ambacho ni muhimu kulinda haki ya zabuni ya Qatar na mawakili wanne wapo tayari kuangalia jambo hili.
"Haki ya kushinda kuandaa mashindano tumeshinda kwa sababu ilikuwa zabuni bora na kwa sababu ni wakati wa Mashariki ya Kati kuandaa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza."
0 Comments