Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capt.Mstaafu Asseri Msangi akifunga Warsha ya siku Mbili ya Wadau wa Utalii Kanda ya Kusini mwa Tanzania.

Na Gabriel Kilamlya.

Mkoa wa Njombe umetoka na Maazimio mbalimbali ya kuweza kukuza na Kuboresha sekta ya Utalii Nchi pamoja na Kukuza Uchumi katika Taifa.

Miongoni mwa Maazimio hayo ni pamoja na kuangalia Vivutio vya kuvipa kipaumbele katika Wilaya zote Mkoani Njombe na Hivyo kuzifanyia Mchakato wa Kuviboresha katika Kukuza Uchumi na Pato la Taifa.



Akitangaza Maazimio hayo Wakati wa Kufunga Warsha ya Siku Mbili ya Sekta ya Utalii iliyokuwa Ikifanyika Mkoani Njombe Afisa Nyuki wa Mkoa wa Njombe bwana Daudi Kumburu amesema kuwa baadhi ya Vivutio hivyo ni pamoja na Maeneo ya Kihistoria ya Mdandu,Msitu wa Nyumbanitu na Kila Wilaya inatakiwa kutenga vivutio vyake na kuvifanyia Kazi.
Akifunga semina hiyo ya Siku Mbili iliyowakutanisha wadau wa Utalii kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Njombe pamoja na wadau kutoka Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mkuu wa mkoa wa Njombe ameagiza wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafakisha kukuza vivutio vilivyobainishwa kila Wilaya huku Maafisa Utalii waliopo na watakao ajiriwa wabainishe mikakati hiyo na kuifikisha kwenye Mabaraza ya Madiwani.


Pamoja na Mambo mengine Captain Msangi amewataka watanzania Kujenga mazoea ya kuibua Vivutio tofauti na Mahotel yaliyozoeleka kama Kujenga ZOO za Wanyama Mkoani Njombe.