MECHI ZOTE AMBAZO MESSI AMEFUNGA KATIKA CHAMPIONS LEAGUE - BARCELONA HAIJAFUNGWA

Leo Messi alifunga goli lake la 51 katika ligi ya mabingwa wa ulaya jana jumanne. Mpaka sasa amefunga magoli 14 katika msimu huu wa ligi ya mabingwa.

Muargentina huyo sasa yupo nyuma ya goli moja tu kuweza kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa Champions league.

Messi sasa anashika nafasi ya tatu katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa champions league, akiwa mbele ya Thierry Henry, na nyuma ya Raul aliyefunga magoli 71 na Van Nisterlrooy aliyefunga 56.

MESSI AKIFUNGA BARCA HAWAFUNGWI
Messi amefunga katika mechi 32 katika champions league, kati ya mechi hizo Barca wameshinda 28 na kutoa sare 4. Katika magoli yake 51, 27 ameyafunga katika uwanja wa Nou Camp, 23 ameyafunga katika viwanja vya ugenini - mawili katika fainali za champions league dhidi ya Manchester United moja jijini Rome na lingine Wembley.

PHOTOS: SIMBA ILIPOWASILI MJINI SETIF - ALGERIA - YAFIKIA HOTEL YA ZINEDINE ZIDANE

Kocha wa Simba Milovan akiwa na daktari wa simba.




Hotel waliyofikia Simba hapa Setif inayoitwa jina la mwanasoka bora wa dunia wa zamani Zinedine Zidane ambaye ana asili ya Algeria

Victor Costa Jumba akiwa na mmoja ya viongozi wa msafara huo

Bwana Salum Machaku akiwa anashangaa shngaa watoto wa kiarabu.

Emmanuel Okwi na Uhuru Suleiman

Ally Mustapha Barthez akiwa na Amiri Maftaa na Felix Sunzu leo walipowasili mjini Setif -Algeria

SIMBA WASTUKIA HUJUMA YA ES SETIF - WAYAKATAA MAJI WALIYOPEWA

Aden Rage akikagua maji hayo kabla ya kuyakataa. Maji hayo yaliletwa na viongozi wa klabu ya ES Setif.

Rage akisisitiza kutoyataka maji yaliyoletwa na ES Setif kwa kuhofia hujuma dhidi ya waarabu hao.

Mtanzania ambaye ni daktari Elihuruma alikuwepo kutoa sapoti kwa Simba huko nchini ya Algeria.

Viongozi wa klabu ya ES Setif wakijadiliana baada ya viongozi wa Simba kugoma kuchukua maji yao waliyoleta.